Connect with us

Makala

Chico Ushindi Atemwa Yanga,Yacouba Hatihati

Klabu ya Yanga sc imetangaza kuachana na winga Chico Ushindi kutokana na kuzidisha idadi ya wachezaji wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu nchini kutoka shirikisho la soka (Tff) na bodi ya ligi nchini ambazo hutaka idadi ya wachezaji wa kigeni isizidi 12 kwa timu moja.

Awali Yanga sc ilikua na mpango wa kusalia na Chico Ushindi ambae ilimsajili kwa  kutokea klabu ya Tp Mazembe lakini aliathiriwa kwa kiasi kikubwa na majeraha kutokana na kutokua Fit kwa sababu ya kutocheza muda mrefu hivyo inaachana nae ili kukidhi matakwa ya kikanuni kutokana na kufanya usajili wa wachezaji wapya kama Benard Morrison,Lazarus Kambole,Ki aziz ambao kwa kiasi kikubwa pia hucheza nafasi moja na winga huyo.

Pia klabu hiyo inaangalia kwa ukaribu mkataba wa Yacouba Songne ambae nae amekua na majeraha ya muda mrefu hivyo klabu itakaa naye kujadili mstakabari wake ambapo kuna mpango wa kumtoa kwa mkopo kwenda klabu ya Geita Gold Fc.

Yanga sc imekamilisha usajili wa wachezaji wapya wa ajili ya msimu ujao ambapo mpaka sasa ina mastaa 12 wa kigeni wakiongozwa na kipa Djigui Diara,Djuma Shabani,Joyce Lomalisa,Yannick Bangala,Khalid Aucho,Jesus Moloko,Heritier Makambo,Fiston Mayele,Benard Morrison,Stephane Aziz Ki,Lazarus Kambole na Gael Bigirimana.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala