Connect with us

Makala

Rasmi Kambi Yanga sc Avic Town

Klabu ya Yanga sc imethibitisha kuwa kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini itafanyika katika eneo la Avic Town yalipo makazi yao ya siku zote badala ya kwenda nje ya nchini kama ilivyokua imepangwa awali ambapo walipanga kwenda nchini Uturuki.

Taarifa za ndani za klabu hiyo zinadai kuwa licha ya kuwa maandalizi ya awali ikiwemo kutafuta hoteli na viwanja vya mazoezi tayari zilishafanyika na uongozi wa klabu hiyo uko tayari kulipa fidia ya hasara hizo lakini lazima ihakikishe inatekeleza ushauri wa kocha mkuu wa klabu hiyo Nasredine Mohamed Nabi ambaye amegomea kambi ya nje ya nchi kutokana na changamoto mbalimbali watakazo kutana nazo ikiwemo suala la muda kutokua rafiki.

Msimu uliopita klabu hiyo iliweka kambi nchini Morroco lakini ilipata changamoto ya kutokua na wachezaji kamili kwa wakati ambapo pia walikutana na changamoto ya ugonjwa wa Corona na kuwalazimu kurudi nchini hali iliyowagharimu katika michezo ya ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United ambapo Yanga sc walitolewa katika hatua hiyo ya awali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala