Kinda wa klabu ya Simba Sc Ladack Chasambi amekua mwiba mkali kwa Kagera Sugar akiiongoza klabu yake kupata ushindi wa mabao 5-2 katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini uliofanyika katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
Katika mchezo huo Chasambi alifanikiwa kupika mabao mawili ambapo wafungaji kwa upande wa Simba sc ni Shomari Kapombe aliyefunga bao la kwanza huku Charles Ahoua akifunga bao la pili dakika chache kabla ya mapumziko.
Fabrice Ngoma aliongeza bao la tatu kwa Simba sc dakika ya 55 ya mchezo akipokea pasi nzuri ya Chasambi huku uamuzi wa kocha Fadlu Davis kumuanzisha Steven Mukwala ulimlipa baada ya mshambuliaji huyo kufunga mabao mawili dakika za 66 na 85 za mchezo huo.
Hata hivyo ushindi huo ulianza kuingia doa baada ya Simba Sc kukubali kufungwa mabao mawili kupitia kwa Datius Peter na Cleophas Mkandala na kufanya dakika 90 kukamilika kwa 5-2.
Simba sc katika mchezo huo ilianza kumtumia kiungo mshambuliaji wake Ellie Mpanzu kwa mara ya kwanza tangu imsajili ambapo alijitahidi kuonyesha kiwango kizuri hasa kasi eneo la mbele.
Chasambi ambaye hakua na mwanzo mzuri klabuni hapo sasa ameanza kupata nafasi ya kuanza baada ya kuimarisha kiwango chake na kuanza kumvutia kocha Fadlu Davis.
Simba sc sasa imefikisha alama 34 kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ikiwa imecheza michezo 13 mpaka katika ligi kuu nchini.