Connect with us

Makala

Camara Nje Guinea Ikiivaa Uganda

Kipa wa klabu ya Simba Sc Moussa Pinpin Camara ameanzia benchi katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la Dunia mwaka 2026 baina ya Taifa lake Guinea dhidi ya Uganda.

Dalili za kipa huyo kutocheza mchezo zilianza kuonekana tangu jana ambapo alishindwa kufanya mazoezi ya mwisho na kikosi cha Guinea kujiandaa na mchezo huo wa leo.

Camara alifanya mazoezi na wenzake kujiandaa na mchezo uliopita dhidi ya Somalia na alikaa benchi kwa dakika zote 90 Za mchezo huo.

Katika mchezo wa leo kocha Michel Dussuyer raia wa ufaransa amemuanzisha kipa Somaila Sylla anayeichezea klabu ya Stade de Reims na kumuacha kipa huyo wa Simba sc akianzia benchi.

Camara aliumia katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Klabu ya Azam Fc uliomalizika kwa sare ya 2-2 ambapo tangu hapo hajacheza mchezo wowote wa mashindano.

Awali madaktari wa timu yake ya Taifa walimuomba ajiunge na kikosi hicho ambapo wamejitahidi kumtibia bila mafanikio makubwa.

 

Kesho uwezekano wa Camara kucheza ni mdogo sababu hajafanya mazoezi ya mwisho na wenzake

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala