Connect with us

Makala

Ali Hassan Mwinyi Yafunguliwa na TFF

Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limeufungulia uwanja wa Ali Hassan Mwinyi uliopo mkoani Tabora baada ya kufanyiwa marekebisho kwa mujibu wa kanuni na sheria za mpira wa miguu nchini.

Awali TFF iliufungia uwanja huo kutokana na kuwa na mapungufu kadhaa ikiwemo eneo la kuchezea kutoa na ubora unaotakiwa ambapo iliwalazimu wamiliki wa uwanja kufanya Marekebisho hayo.

Taarifa iliyotolewa na TFF inasema kuwa uwanja huo umefunguliwa rasmi kutumika katika michezo ya ligi kuu baada ya kufanyiwa marekebisho ambapo baada ya timu ya ukaguzi kujiridhisha sasa umefunguliwa rasmi.

Taarifa hiyo imekua neema kwa wana Tabora ambao sasa wataiona timu yao ya Tabora United ikirejea uwanjani hapo baada ya kuhama kutokana na kufungiwa kwa uwanja huo.

Tabora United itacheza na Yanga sc katika mchezo ujao wa ligi kuu ya Nbc ambao unatarajiwa kuwa mkali kutokana na ubora wa Tabora United ambao mchezo wa awali waliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala