Haidhaniwi kama itapata ushindi katika mchezo wa marudiano dhidi ya Usm Algers baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 katika mchezo wa fainali ya kwanza ya kombe la shirikisho barani Afrika uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.
Yanga sc ikianza bila staa wa eneo lake la kiungo Khalid Aucho ilikubali kutawaliwa katika eneo hilo huku uwepo wa Aziz Ki ambaye hakua na mchezo mzuri ukizidisha ugumu kwa Yanga sc ambao waliruhusu bao la kwanza kwa kichwa cha Aymen Mahious dakika ya 32 ya mchezo.
Mwalimu Nabi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Tuisila Kisinda,Aziz Ki na Dickson Job pamoja na Kibwana Shomari na kuwaiungiza Djuma Shabani,Joyce Lomalisa,Benard Morrison na Salum Abubakar hali iliyosababisha Yanga sc kutawala mchezo na kupata bao la kusawazisha dakika ya 82 kupitia kwa Fiston Mayele.
Dakika mbili baadae Usm Algers walipata bao la pili kutokana na walinzi wa Yanga sc kukosa nidhamu ya kujilinda na kusababisha bao hilo lililofungwa na Islam Merili na kuwazima wananchi.
Yanga sc sasa inalazimika kushinda kuanzia mabao mawili ugenini katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Juni 3 mwaka huu huku wakizuia kutofungwa ili kujihakikishia ubingwa wa kombe hilo la pili kwa ukubwa kwa ngazi za klabu barani Afrika.