Connect with us

Kikapu

Bosi Simba sc Afafanua Kuhusu Posho

Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Simba sc Iman Kajula amefafanua kuhusu madai ya klabu hiyo kudaiwa posho na wachezaji wa klabu hiyo hali iliyosababisha kupoteza mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Azam Fc.

Simba sc ilipoteza kwa mabao 2-1 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara huku taarifa zikisambaa kwa kuna mgomo baridi miongoni mwa wachezaji kutokana na madai yao ya posho za michezo mbalimbali.

Madai hayo yalithibitishwa na Ahmed Ally meneja wa habari wa klabu hiyo lakini imemlazimu bosi huyo kujitokeza na kutoa ufafanuzi kuhusu madai hayo.

“Timu yetu imeshatoa Bonus zaidi ya Billion 1.1 na kiasi kilichobaki ni milioni 20 pekee tena ni Bonus ya Ligi ya ndani, wewe vuta picha Klabu inalipa zaidi ya Billion 1.1 inashindwaje kulipa milioni 20 haingii akilini hilo ni jambo linalopitia mchakato wa kitaasisi na lipo ndani ya uwezo wetu”.

Pia Kajula aliendelea kusema kuwa “Vuta picha wachezaji wanalipwa mshahara kiasi gani na ukilinganisha na milioni 20 ambayo watagawana watu zaidi ya 30 kila mmoja atapata kiasi gani, ambapo kukosekana kwake ije iathiri matokeo kwenye mechi.””- Imani Kajula Mtendaji Mkuu Simba SC.

Pia Mtendaji Mkuu Iman Kajula, amesema kwenye mikataba yao hakuna sehemu ambayo imesema itawalipa Bonus ila huwa wanatoa kwa ajili ya kuwahamasisha wapandane zaidi kwenye kile wanachokipambania.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Kikapu

  • Yanga sc Hali Tete

    Haidhaniwi kama itapata ushindi katika mchezo wa marudiano dhidi ya Usm Algers baada ya...

  • Nabi Yupo Sana Yanga sc

    Baada ya tetesi za muda mrefu kuwa anaweza kuondoka klabu hapo kocha wa Yanga...

  • Worriars Mambo Magumu

    Timu ya Golden State Warriors, imeendelea kufanya vibaya msimu huu baada ya kukubali kichapo...