Connect with us

Kikapu

Nabi Yupo Sana Yanga sc

Baada ya tetesi za muda mrefu kuwa anaweza kuondoka klabu hapo kocha wa Yanga sc Nasreddine Nabi amesaini mkataba mpya wa kusalia klabuni hapo kwa miaka miwili zaidi.

Nabi amesaini mkataba huo na kuzipiga chini ofa alizokuwa nazo kutoka klabu zenye hela za Far Rabat ya nchini Morroco na Al Hilal ya Sudan ambazo zilionyesha nia ya kumsajili.

Taarifa za ndani zinasema kwamba Nabi ameamua kubakia Yanga sc akiamini kuwa kutokana na uwekezaji uliofanywa kikosini humo anaweza kufanya makubwa katika ligi ya mabigwa barani Afrika ambayo klabu hiyo inashiriki msimu huu.

Mbali na kukubali kusaini mkataba mpya pia maslahi ya kocha huyo yameongezeka kwa kiasi kikubwa huku ikisemekana atapokea zaidi ya milioni 30 za kitanzania kwa mwezi

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Kikapu