Worriars Mambo Magumu

0

Timu ya Golden State Warriors, imeendelea kufanya vibaya msimu huu baada ya kukubali kichapo cha pointi 108-114 dhidi ya timu ya Oklahoma Thunder.

Licha ya nyota mpya wa Warriors, D’Angelo Russell, kufunga pointi 30 lakini hazikutosha kuiepusha na kipigo kutoka kwa Oklahoma.

Warriors wameonekana kufanya vibaya msimu huu, baada ya kuwakosa nyota wao watatu, Stephen Curry, Draymond Green na Klay Thompson, ambao wote ni majeruhi huku Curry akikosa mechi zote zilizosalia za msimuu huu huku siku ya alhamisi watakua ugenini kuvaana na L.A lakers.

Leave A Reply

Your email address will not be published.