Bondia wa Uingereza mwenye asili ya Nigeria Anthony Joshua amepoteza pambano lake la uzito wa juu la kugombania mikanda dhidi ya bondia wa Ukrane Aleksandr Usyk katika pambano lilifanyika usiku wa kuamkia leo jijini London.
Pambano hilo lililohudhuriwa na watazamaji zaidi ya 65,000 katika uwanja wa Tottenham Hotspur wameshuduhia Joshua akivuliwa ubingwa wa WBO na mshindani wake huyo ambaye ni bingwa wa zamani wa uzito wa kati.
Joshua alitazamiwa kupigana na bondia mwenzie wa Kiingereza Tyson Fury mwezi uliopita lakini pambano lao liliahirishwa kutokana na sababu za ugonjwa wa Uviko-19,ndipo Joshua akaamua kupambana na Usyk ambaye alipaswa kutetea ubingwa wa WBO dhidi yake.
Usyk alikuwa na mchezo mzuri katika pambano hilo ambapo alifanikiwa kushinda kwa pointi 117-112,116-112,115-113 kutoka kwa majaji katika raundi12,huku akimfanya AJ kucheza kwa kutumia jicho moja muda mrefu wa pambano hilo.
Hata hivyo licha ya kupoteza ubingwa wake Anthony Joshua amesema kuwa bado atambana na Tyson Fury bila hata mkanda kwani nia yake ya kumtandika bondia huyo bado iko palepale.
Usyk amebeba mikanda yote mitatu ya WBA,IBF na WBO iliyokuwa ikishikiriwa na AJ,hata hivyo kuna uwezekano wa pambano la marudiano baina ya mabondia hao kwa mujibu wa mkataba waliosaini.