Connect with us

Makala

Yanga sc Yalipa Kisasi

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kulipa kisasi cha kuvunjiwa rekodi yake ya kutofungwa michezo 49 baada ya kuifunga timu ya Ihefu Fc 1-0 katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Yanga sc iliingia katika mchezo huo bila ya mastaa wake kadhaa wa kikosi cha kwanza kama ilivyo siku zote ambapo iliwakosa Yannick Bangala,Khalid Aucho,Benard Morrison,Aziz Ki na Feisal Salum huku ikimuanzisha kwa mara ya kwanza mchezaji Mudhathir Yahya Abbass eneo la kiungo aliyeshirikiana na Salum Abubakar/

Ihefu ikiwa na mastaa wake wakiongozwa na Juma Nyosso,Obrey Chilwa,Never Tigere,Nico Wadada na wengineo ilishindwa kufua dafu mbele ya Yanga sc iliyokua na uimara eneo la kiungo japo eneo la ushmbuliaji lilikosa ufanisi hasa kutokana na Tuisila Kisinda kutokua makini katika kutumia nafasi za mabao mara kadhaa.

Makosa binafsi ya Kipa Fikirini Bakari dakika ya 64′ ya mchezo yalisababisha Yanga sc kupota bao lililofungwa na Fiston Mayele bao mablo lilidumu mpaka dakika 90 za mchezo huo ambao pia ulimtambulisha rasmi Kennedy Musonda kama usajili mpya wa klabu hiyo akipewa jezi namba 25.

Yanga sc sasa imefikisha alama 53 kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini huku ikiwa na michezo 20 ya ligi kuu na ikisaliwa na michezo10 ili ligi itamatike.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala