Connect with us

Makala

Metacha,Beki Kisiki Watambulishwa Yanga sc

Klabu ya Yanga sc imewatambulisha wachezaji Metacha Mnata na Seydou Doumbia kama wachezaji wapya wa klabu hiyo baada ya kuwasajili dakika za lala salama za dirisha la usajili nchini siku ya Januari 15 usiku saa sita kamili.

Yanga sc imelazimika kumsajili Metacha Mnata iliyomtema miaka miwili iliyopita baada ya kuwa na matatizo ya utovu wa nidhamu ili kuziba nafasi ya Aboutwalib Mshery ambaye amepata majeraha ya goti na anatarajiwa kuwa nje kwa muda mrefu akijiuguza majeraha hayo.

Pia usajili wa Doumbia 27′ umefanyika kwa lengo hasa la michuano ya kimataifa kutokana na beki huyo kuwa na uzoefu mkubwa katika michuano hiyo akiwa kama nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya wachezaji wa ndani wa Mali inayoshiriki katika michuano ya Chan nchini Algeria.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala