Connect with us

Makala

Nabi Alia na Waamuzi

Kocha wa klabu ya Yanga sc Nasredine Nabi amelia na kiwango cha waamuzi waliochezesha mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba sc ambao timu yake ilipoteza kwa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Yanga sc ilikubali kipigo cha pili katika ligi kuu msimu huu baada ya kufungwa kwa mara ya kwanza na Ihefu Fc jijini Mbeya mwishoni mwa mwaka jana na sasa imefungwa kwa mara ya pili na kufanya tofauti ya alama kusalia tano kutoka nane katika msimamo wa ligi kuu msimu huu.

Nabi alisema maneno hayo wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo huo ” Goli la kwanza tulilofungwa halikuwa halali kwasababu ile haikutakiwa kuwa kona,walioangalia kwenye TV watakuwa wameona”.

“Unapofungwa bao la haraka kama vile ndani ya dakika 05 za kwanza inakutoa mchezoni hasa linapokuwa bao lisilostahili kipindi cha pili tulirudi vyema lakini Simba walikuwa bora kulinda ushindi na pongezi kwao “.

Yanga sc sasa imesaliwa na michezo minne muhimu ambapo ikishinda miwili na kutoa sare mchezo mmoja itakua imetangaza  ubingwa wa ligi kuu nchini kwa mara ya 29.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala