Connect with us

Soka

EPL yatangaza likizo kombe la dunia Qatar 2022

Bodi ya ligi nchini Uingereza(premier league) imetangaza kuwa kutakuwa na mapumziko mafupi ya ligi kuu kuanzia Novemba 14 wiki moja kabla ya kuanza kwa kombe la dunia 2022 nchini Qatar na ligi itarejea Desemba 26 baada ya kumalizika kwa michuano hiyo.

Kombe la dunia Qatar 2022 litakuwa ni la kwanza katika historia ya michuano hiyo kuchezwa mwishoni mwa mwaka tofauti na ilivyozoeleka kufanyika mwezi Juni tangu kuanzishwa kwake mwaka 1934.

Likizo hiyo ni kwaajili ya kutoa nafasi kwa wachezaji kwa wachezaji wanaoshiriki ligi kuu na ligi daraja la kwanza kwenda kuzitumikia timu zao za Taifa zitakazokuwa zinashiriki michuano hiyo mikubwa zaidi duniani.

Mapumziko hayo ni kwa msimu wa 2022/2023 ambao utaanza rasmi Agosti 6 mwakani na kumalizika Mei 28 2023,msimu huo utakuwa na raundi 34 za mechi kuchezwa mwisho wa juma,raundi 3 za katikati ya juma na raundi moja kwenye siku likizo ya Benki(Bank holiday) na mechi za mzunguko wa 16 kati ya Novemba 12 na 13 ndio zitakuwa za mwisho kabla ya mapumziko hayo kuanza.

Msimu huo ndio utakuwa msimu pekee kwenye historia tangu ianze kuitwa ‘premier league’ kwa raundi nyingi(34) kuchezwa wikiendi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka