Connect with us

Soka

Dani arejea Barca

Beki mkongwe wa kulia Dani Alves anarejea tena kwa mara ya pili kuitumikia klabu ya soka ya Fc Barcelona baada ya usajili wake kuidhinishwa na kocha mkuu mpya wa timu hiyo Xavi Hernandes.

Dani kwasasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Sao Paulo ya kwao Brazil kuisha mwishoni mwa msimu uliopita.

Makubaliano baina ya Barcelona na kambi ya Alves yamefikiwa hii leo na kukubaliana mkataba wa mwaka mmoja kuichezea tena timu hiyo aliyopata nayo mafanikio makubwa,usajili wake unasubiriwa tu kuthibitishwa na la liga kabla ya kutangazwa rasmi.

Beki huyo mwenye miaka 38 anarejea Barcelona kuongeza hamasa ndani ya uwanja na katika vyumba vya kubadilishia nguo vya timu hiyo iliyojaa damu changa nyingi,huenda akajiunga rasmi na benchi la ufundi la klabu hiyo chini ya Xavi mkataba wake utakapotamatika.

Dani Alves alijiunga na Barcelona mwaka 2008 akitokea Sevilla na kuhudumu hadi mwaka 2016 alipotimkia Juventus ya Italia,akiwa Camp Nou ametwaa mataji 6 ya la liga,4 ya kombe la Mfalme(Copa Del Rey),3 ligi ya mabingwa Ulaya,3 klabu bingwa dunia,3 ngao ya hisani.

Mchezaji huyo ndiye anatajwa kuwa mchezaji aliyetwaa mataji mengi zaidi duniani akichukua mataji 43 tangu aanze kucheza soka la kulipwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka