Connect with us

Soka

Vilabu EPL vyakataa kombe la dunia

Vilabu vyote 20 vinavyoshiriki ligu kuu soka nchini Uingereza kwa pamoja vimepiga kura ya kupinga mpango wa FIFA kuandaa michuano ya kombe la dunia kila baada ya miaka miwili(Biennial world cup).

Mpango huo ulipendekezwa na mkurugenzi wa maendeleo FIFA katika masuala ya kiufundi mzee Arsene Wenger kocha wa zamani wa Arsenal.

FIFA ilipanga kuleta wazo hilo kuanza kufanya kazi baada ya kombe la dunia Qatar 2022,lakini wadau wengi wa soka wamekuwa wakilipinga kwa kile wanachodai kuwa litaharibu radha na hadhi ya michuano hiyo lakini pia litalita muingiliano mkubwa wa ratiba za kimashindano kote ulimwenguni.

Siku ya jana nchi ya Uingereza imepiga kura rasmi kuukata mpango huo huku wakiuona mpango huo kuwa ni wa kibiashara zaidi wakiufananisha na ule wa European super league.

Wenger amesema hakuna haja ya kuwa na wasiwasi na mpango huo,mashabiki wa soka duniani wanapaswa kupewa elimu juu ya hili na sio kutumia sababu za kihisia kuamua,watu waelevu siku zote huhoji,hupima viwango na kuangalia mambo kwa mtazamo mkubwa zaidi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka