Connect with us

Makala

Banda Kuvuna Mamilioni Richard Bay

Beki Mtanzania Abdi Banda anajiandaa kupokea Mamilioni kutoka katika Klabu ya Richard Bay inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika ya kusini baada ya kushinda kesi yake dhidi ya klabu hiyo.

Banda alifungua kesi katika Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kupitia combo chake maalumu cha kusimamia malalamiko ya mikataba kwa wachezaji ambapo iliamuriwa klabu hiyo imlipe Staa huyo kiasi cha shilingi milioni 360 za kitanzania.

Fifa katika kukazia hukumu hiyo imeifungua klabu hiyo kufanya usajili wa wachezaji wapya mpaka pale itakapomlipa staa huyo ambaye kwa sasa anaichezea Dodoma Jiji Fc kwa mkataba wa miezi sita.

Hii si mara ya kwanza kwa Banda kulipwa Mamilioni ambapo msimu uliopita alilipwa takribani kiasi cha shilingi milioni 180 baada ya klabu ya Chipa United kuvunja mkataba na staa huyo.

Banda tangu aachane na Simba sc amekua hatulii katika timu nyingi hasa za nje ya nchi ambapo alizichezea klabu za Baroka Fc,Chipa United,Mtibwa Sugar na Dodoma Jiji.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala