Klabu ya Yanga sc imezidi kunogesha safari yake ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Klabu bingwa barani Afrika baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Klabu ya Tp Mazembe katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam Siku ya Disemba 5 2024.
![](https://sportsleosw.com/wp-content/uploads/2025/01/FB_IMG_1736182520952.jpg)
Wadau wa soka nchini walishaanza kukata tamaa juu ya klabu hiyo kuingia hatua hiyo baada ya kupoteza michezo yake miwili ya awali wakifungwa mabao 2-0 dhidi ya Al Hilal Fc jijini Dar es Salaam na pia walipoteza kwa mabao hayo hayo dhidi ya Mc Algers ugenini.
Kisha Yanga sc iliyokua imetoka kubadili kocha ililazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Klabu ya Tp Mazembe ugenini kwa bao la jioni la Prince Mpumelelo Dube na kuanza kupiga hesabu zake sawa huku ikiwa mkiani na alama moja.
Kitendo cha kupata ushindi huo wa mabao 3-1 umerudisha matumaini kwa mashabiki na wadau wa soka nchini ambapo sasa klabu hiyo imefikisha alama nne ikiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo huku sare ya 1-1 ya Al Hilal dhidi ya Mc Algers ikizidi kuweka matumaini makubwa ya kufuzu.
Msimamo wa kundi A unasoma Al Hilal ipo kileleni na alama 10 huku Mc Algers wakiwa na alama sita na Yanga sc ina alama nne huku Mazembe ikishika mkia na alama mbili.
![](https://sportsleosw.com/wp-content/uploads/2025/01/FB_IMG_1736182551930.jpg)
Hata hivyo Yanga sc inapaswa kushinda mchezo mgumu unaofuata nchini Mauritania dhidi ya Al Hilal Fc ili kutengeneza mazingira mazuri ya kufuzu huku ikiombea Mc Algers ifungwe ama itoe sare ili hatma ya mshindi wa pili wa kundi hilo iamriwe katika mchezo wa mwisho katika uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Mc Algers.
Katika mchezo huo Yanga sc ilipata mabao yake kupitia kwa Clement Mzize aliyefunga mawili huku Stephan Aziz Ki akifunga bao moja na Tp Mazembe walitangulia kupata bao la mapema la penati.