Connect with us

Soka

Yanga sc Yaizamisha Mtibwa Sugar

Klabu ya Yanga sc imerudi kwa kasi katika ligi kuu nchini baada ya kuibamiza Mtibwa Sugar kwa mabao 4-1 na kuendelea kujiwekea mazingira mazuri ya kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya soka ya NBC hapa nchini.

Yanga sc iliingia katika mchezo huo ikiwa na mabadiliko kadhaa katika kikosi cha kwanza ambapo Nickson Kibabagee,Salum Abubakari,Jesus Moloko,Mahaltse Makudubela na Kibwana Shomari walianza katika mchezo huo baada ya mwalimu Miguel Gamondi kuamua kupumzisha baadhi ya mastaa.

Mtibwa Sugar kama kawaida iliyokua na vijana wengi kutoka kikosi chake cha umri wa miaka 20 ambapo zaidi ya vijana watano wamepandishwa kikosi cha wakubwa ambapo kutokana na uchanga huo walishindwa kuhimili mziki wa Yanga sc na kuruhusu bao la kwanza kwa penati likifungwa na Stephane Aziz Ki kwa tuta baada ya Clement Mzize kuangushwa eneo la hatari mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

Aziz Ki tena dakika ya 65 alimalizia kazi nzuri ya Kibwana Shomari na kufanikiwa kuandika bao la pili katika mchezo huo huku likiwa ni bao lake ya tisa katika ligi kuu nchini akiwachambua walinzi wa Mtibwa Sugar huku dakika 11 baadae Kennedy Musonda aliandika bao la tatu kwa shuti kali akimalizia kazi ya Jesus Moloko.

Skudu alifanikiwa kuandika bao lake la kwanza katika mchezo huo akifunga kwa shuti kali dakika ya 83 ambalo lilimshinda kipa wa Mtibwa Sugar.

Seif Karihe alitumia akili kubwa akimsoma Djigui Diarra ambaye alitoka golini na kufanikiwa kuipatia Mtibwa Sugar bao la kufutia machozi dakika ya 90+4.

Baada ya matokeo hayo Mtibwa Sugar imezidi kuzama  mwishoni mwa msimamo wa ligi kuu nchini ikiwa na alama tano tu katika michezo 13 ya ligi kuu nchini huku Yanga sc wakiwa katika nafasi ya pili ya msimamo wakiwa na alama 27 katika michezo 10 ya ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka