Connect with us

Soka

Yanga SC yaanza vibaya klabu bingwa

Klabu ya soka ya Yanga imeanza vibaya michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya kupoteza kwa goli 1-0 nyumbani dhidi ya Rivers United ya Nigeria katika mchezo wa kwanza wa hatua za awali za mtoano.

Yanga ilianza mchezo huo kwa kasi wakionesha kuhitaji matokeo ya haraka kwa kutengeneza nafasi ambazo hata hivyo hawakuweza kuzitumia vizuri.

Kipindi cha upepo ulibadilika ambapo safari hii ni Rivers ndio waliutawala zaidi mchezo na kufanikiwa kupata goli pekee la mchezo dakika ya 51 kupitia kwa mshambuliaji Moses Omodumuke aliyeunganisha kwa kichwa baada ya mabeki wa Yanga kuzubaa.

Yanga sasa ina mlima mkubwa wa kupanda kupindua matokeo katika mchezo wa marudiano utakaofanyika wiki ijayo nchini NIgeria.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka