Connect with us

Makala

VAR Kutumika Ligi Kuu 2024

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi kuu nchini Tanzania Almas Kasongo amesema kwamba kuanzia msimu ujao wa ligi kuu ya Nbc nchini mfumo wa mwamuzi msaidizi wa Video (Video Assistant Referee) utaanza kutumika katika michezo mbali mbali ya ligi kuu.

Kasongo amesisitiza hayo wakati akifanyiwa mahojiano na Shirika la Habari nchini Tanzania (Tbc) ambapo amesema kuwa maandalizi yapo tayari kwa ajili ya kufunga mitambo hiyo huku tayari mafunzo yameshaanza kutolewa kwa waamuzi wasaidizi watakaoendesha mitambo hiyo.

“Tutakuwa na VAR na tutaanza na michezo kadhaa ambayo utaratibu wake utatengenezwa na Kamati ya maamuzi na wataalamu na tutajitahidi kila timu iwe sehemu ya mechi zake kuamuliwa na hio teknolojia, wataalamu na waamuzi wanaendelea na mafunzo”.Alisema Kasongo

Pia alisisitiza kuwa VAR itatumika katika baadhi ya viwanja na sio vyote vya ligi kuu kutokana na utofauti wa miundombinu huku baadhi ya viwanja ikiwa ni ngumu kufunga mitambo hiyo.

“Haitakuwa kwenye viwanja vyote itakuwa baadhi ya viwanja kuna baadhi ya VAR zitakuwa mobile tutakuwa na siku maalumu ya kuelezea ,safari moja huanzisha nyingine”.Alimalizia kusema Mtendaji huyo mkuu wa kwanza tangu bodi hiyo ianzishwe.

VAR tangu ianzishwe duniani imekua na mwitikio mkubwa ambapo ligi kubwa ulaya na barani Afrika karibia zote sasa zinatumia mfumo huo ili kuboresha zaidi utoaji wa haki katika mpira wa miguu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala