Connect with us

Makala

Waziri Jr Atimkia Dodoma Jiji

Mshambuliaji Waziri Junior ameisaini katika klabu ya Dodoma Jiji FC kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea KMC FC ambapo amemaliza mkataba wake msimu huu ulioisha wa ligi kuu.

Awali Pamba Jiji FC ilionesha nia ya kumsajili Waziri Junior na ikamtumia hadi nauli ya kwenda jijini Mwanza kusaini mkataba wa Pamba Jiji FC ila hakwenda na badala yake akasaini Dodoma Jiji FC, baada ya kuvutiwa na ofa yao nono.

Waziri nje na timu hiyo pia amepata ofa nono nchini Qatar ambapo kuna timu ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza imevutiwa na uwezo wa mshambuliaji huyo huku kukiwa na urahisi zaidi kuvunja mkataba wake na Dodoma Jiji kutokana na kuwepo na kipengele cha kumruhusu kuondoka iwapo atapata timu nje ya nchi.

Waziri ni moja ya washambuliaji hatari wazawa nchini ambapo ana uwezo mkubwa zaidi wa kufunga mabao makali huku msimu huu ulioisha akiwa na Kmc alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 12 katika ligi kuu ya soka ya Nbc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala