Home Soka Kijiri Atua Simba Sc

Kijiri Atua Simba Sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imekamilisha usajili wa beki Kelvin Kijiri aliyekua Singida Black Stars kwa mkataba wa miaka miwili ambapo sasa yupo njiani kujiunga na timu hiyo iliyoko kambini nchini Misri.

Kijiri anaungana na mabeki Shomari Kapombe na David Kameta kuunda jeshi kamili la Simba sc kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu huku beki Israel Mwenda akiondoka kikosini humo.

Mwenda anatajwa kwenda Singida Big Stars akipishana na Kijiri ambapo sasa anakwenda kupata uhakika wa kucheza mara nyingi tofauti na alipokua Simba sc.

banner

Sababu kubwa ya Mwenda kuondoka klabuni Simba sc inatajwa kuwa moja ni kutokua na uhakika wa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza sambamba na kuwa na maelewano hafifu na Shomari Kapombe.

Simba sc msimu huu imepania kurudisha ufalme wake uliopotea kwa takribani miaka mitatu ambapo sasa imefanya usajili wa maana wa mastaa wa uhakika wa ndani na nje ya nchi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited