Connect with us

Soka

Tpl Mabango 39 Uwanjani

Mtendaji Mkuu wa bodi ya Ligi (TPLB), Almasi Kasongo, amesema msimu ujao wamepanga kuitangaza zaidi Ligi Kuu kwa kuweka mabango 39, uwanjani na timu itakaidi agizo hili itakumbana na adhabu kubwa.

Katika mabango hayo mgawanyo utakua kama ifuatavyo,Timu itayokuwa nyumbani inapaswa kuwa na mabango yake 10 na mdhamini mkuu anapaswa kuwa na mabango 12.

Mabango mengine yanayopaswa kuwa uwanjani, matano kutoka Azam Media na benki ya KCB ambayo ni miongoni mwa wadhamini wataweka mabango manne katika viwanja hivyo vitakavyotumika katika ligi kuu nchini.

“Mabango ya matangazo yanaongeza thamani ya timu hivyo timu zote zinapaswa kujitangaza tofauti na msimu uliopita,Nataka nikumbushe klabu zote sababu kanuni hiyo ilisainiwa hivyo yeyote atakayekaidi atakutana na adhabu kwa mujibu wa sheria”.Alisema mtendaji huyo mkuu wa ligi kuu nchini iliyoanzishwa miaka kadhaa iliyopita.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka