Connect with us

Soka

Tarimba Alia Figisu Uchaguzi TFF

Mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba amelalamika kuhusu utaratibu wa kupata udhamini huku akithibitisha kuwa alikuwa na mpango wa kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF).

Lakini kutokana na mchakato huo kuwa na viashiria vya uvunjifu wa Demokrasi anasita kuchukua fomu hizo kwa hofu ya kukosa wadhamini ambapo kila kanda haiwezi kudhamini wagombea wawili.

Habari za ndani zinadai Licha ya fomu hizo kuanza kutolewa jumanne hii, mchakato wa kutafuta wadhamini umekuwa mgumu kwa kuwa tayari kuna mtu [Karia] ameshazunguka na anaendelea kuzunguka mikoani na kupata udhamini wa wajumbe wote kabla ya mchakato wenyewe kuanza.

Kitaratibu mdhamini hawezi kudhamini wagombea wawili, amesema maswala haya yanatia aibu kwa taifa maana wajumbe wameshaandaliwa kwa ajili ya mtu mmoja.

Cc:Mitandao

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka