Connect with us

Makala

Stars Yainyuka Zambia

Bao pekee la Waziri Junior dakika ya 5 ya mchezo wa kuwania kufuzu kombe la Dunia mwaka 2026 nchini Marekani,Canada na Mexico limeipata timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) alama tatu muhimu katika mchezo dhidi ya Zambia uliofanyika katika uwanja wa Levy Mwanawasa Ndola nchini Zambia.

Waziri alifunga bao hilo akipokea pasi nzuri ya Mudathir Yahya Abbas ambaye alimnyang’anya mpira mchezaji wa Zambia kisha akawahadaa walinzi kabla ya kutoa pasi ya goli kwa mfungaji na kuwashangaza maelfu ya Wazambia waliokua wamefurika katika uwanja huo.

Baada ya goli hilo Zambia wanaonolewa na kocha wa zamani wa Chelsea Avram Grant waliamka na kuanza kupeleka mashambulizi ya nguvu kwa Taifa Stars lakini uimara wa kipa Ally Salim na mabeki wa kati wa Stars Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca ulitosha kuwapa alama tatu Stars.

Zambia ni kama haikua na bahati jioni hiyo baada ya kugongesha mwamba mara mbili huku Patson Daka akikosa nafasi kadhaa za wazi na uamuzi wa timu hiyo kutumia mipira ya juu uligharimu zaidi kutokana na uimara wa Stars kucheza mipira ya juu.

Msimamo wa kundi E sasa Morocco wapo kileleni wakiwa na alama 9 katika michezo mitatu huku Tanzania ikiwa na alama 6 michezo mitatu na Niger ikiwa nafasi ya tatu katika michezo 2 huku Zambia ikiwa nafasi ya nne ikiwa na alama 3 katika michezo minne na Congo ikiwa haina alama licha ya kucheza michezo miwili huku Eritrea ikiwa imejitoa katika michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala