Connect with us

Makala

Stars Yafuzu Chan 2025

Timu ya Taifa ya Tanzania kwa wachezaji wa ndani imefanikiwa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani itkayofanyika nchini mwaka 2025.

Kikosi cha timu hiyo kimefuzu licha ya kupoteza mchezo huo wa marudiano uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza dakika 90 za mchezo huo kwa kushinda bao 1-0 likifungwa na Crispin Ngushi dakika ya 34 na kufanya matokeo ya jumla kuwa 1-1 na mchezo kwenda kwenye hatua ya matuta ambapo Stars ilipoteza mchezo huo kwa penati 5-6 za Sudan.

Kutokana na Tanzania kuwa mwenyeji wa michuano hiyo,imefuzu kushiriki michuano hiyo pamoja na kufungwa na Sudan.

Michuano hiyo itakayofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania ambapo pia ikitumika kama njia ya kufanya tathmini kuona kama nchi itakua tayari kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2027 ambayo utafanyika kwa Ushirikiano wa Tanzania,Kenya na Uganda.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala