Connect with us

Makala

Staa Uganda Anukia Yanga Sc

Klabu ya Yanga Sc imeanza mikakati ya kuimarisha safu yake ya ushambuliaji katika dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Disemba 15 mwaka huu ambapo tayari wameanza mazungumzo na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Fahad Bayo.

Mshambuliaji mwenye umri wa miaka 26, inaripotiwa kuwa ameshafanya mazungumzo na mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania na mazungumzo yamefikia katika hatua nzuri na kinachosubiriwa ni dirisha dogo ilifunguliwe ili nyota huyo ajiunge na Yanga.

Tayari mchezaji huyo yupo katika kambi ya klabu hiyo iliyopo maeneo ya Avic Town akiendelea na mazoezi huku maamuzi ya mwisho kumsajili yanategemea na kocha Sead Ramovic atakavyoamua ambapo kati ya Jean Baleke na Kennedy Musonda mmoja wapo atampisha mshambuliaji huyo.

Kwa sasa, Bayo ni mchezaji huru baada ya kutemwa na MFK Vyskov inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Czech ambayo aliichezea mechi 42 na kuifungia mabao manane. Kabla ya kujiunga na Vyskov, Bayo aliitumikia Ashdod inayoshiriki Ligi Kuu ya Israel ambako katika mechi 41 alizoichezea, alifunga mabao manane huku akipiga pasi moja ya mwisho.

Katika timu ya taifa ya Uganda, mshambuliaji huyo amecheza mechi 21 na kuhusika na mabao tisa, akifunga mabao manane (8) na kupiga pasi moja ya mwisho. Ni mchezaji mwenye uzoefu kutokana na idadi ya klabu alizowahi kuzichezea ndani ya nje ya Afrika ambazo ni MFK Vyskov (Czech), FC Ashdod (Israel) Bnei Sakhnin (Israel), Buildcon FC (Zambia), Vipers (Uganda) na Proline (Uganda)

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala