Connect with us

Makala

Simba Sc Yasogezewa Singida Bs

Bodi ya ligi kuu nchini imefanya mabadiliko madogo katika ratiba ya ligi kuu nchini ambapo klabu ya Simba Sc sasa itapambana na Singida Black Stars siku ya Disemba 28 mwaka huu katika uwanja wa Liti mjini Singida.

Awali ratiba ilikua siku hiyo Simba sc ivaane na Tabora United katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora lakini kutokana na uwepo wa kiporo ikailaziku bodi kuusogeza mechi hiyo mbele ambapo itapangiwa ratiba nyingine.

Simba sc italazimika kujipanga vilivyo kuelekea mchezo huo kutokana na uimara wa wapinzani wao ambao mpaka sasa wana alama 30 wakiwa wamecheza jumla ya michezo 14 ya ligi kuu huku Simba Sc wakiwa na alama 27 katika michezo 11 ya ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala