Connect with us

Soka

Simba sc vs TP Mazembe Simba Day

Mabingwa wa soka Tanzania Bara klabu ya soka ya Simba inatarajia kumenyana na mabingwa wa soka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo klabu ya TP Mazembe katika mchezo wa kirafiki kwenye tamasha lao la Simba day.

Mchezo huo utafanyika tarehe 19 Septemba mwaka huu katika dimba la Benjamini Mkapa kwenye kilele cha tamasha hilo.

Awali Simba kupitia kaimu mkuu wa habari wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga walisema kuwa kwenye Simba day watacheza na timu ya Afrika iliyowahi kutwaa mataji matatu ya klabu bingwa Afrika,hivyo ujio wa Mazembe umethibitisha hilo.

Simba sc kwasasa wapo Arusha wakiendelea na maandalizi ya msimu mpya wa kimashindano pamoja na kuelekea katika mtanange huo wa kirafiki na mabingwa hao mara tano wa klabu bingwa Afrika TP Mazembe.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka