Connect with us

Soka

Samata,Msuva Kuwakosa Malawi

Mastaa wa timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) Mbwana Samata na Saimon Msuva wataukosa mchezo wa kirafiki wa timu hiyo dhidi ya Malawi utakaofanyika siku ya Jumapili kutokana na Sababu mbalimbali.

Wakati Msuva atakuwa na klabu yake [Wydad Casablanca] kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs upande wa Samata yeye atakua na udhuru kutokana na matatizo ya kifamilia yanayomkabili.

Kwa Upande wa meneja wa timu Nadir Haroub Canavaro alisisitiza kuwakosa wachezaji hao huku akisema kuwa maandalizi yanaendelea ”Maandalizi yanaendea, leo kutakuwa na mazoezi asubuhi kwenye uwanja wa Taifa. Kila mchezaji anatamani kucheza mechi ya Jumapili [Tanzania vs Malawi] lakini benchi la ufundi ndio litaamua nani atapata nafasi kwenye mchezo huo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka