Connect with us

Makala

Ronaldo Kumleta Haaland Old Trafford

Mabosi wa usajili wa klabu ya Manchester United wanaamini usajili wa Cristiano Ronaldo klabuni hapo utavutia mastaa wakubwa duniani kuja kujiunga na klabu hiyo ili wapate nafasi ya kucheza na staa huyo maarufu duniani.

Ronaldo 36 alijiunga na Manchester United mwishoni mwa dirisha la usajili akitokea Juventus kwa dau la Paundi milioni 28 na kuikacha klabu wapinzani Manchester City ambao walipewa kipaumbele kumsajili mreno huyo mwenye rokodi wa Guinnes ya kufunga mabao mengi katika timu ya Taifa akifunga mabao 111 mpaka sasa.

Mabosi hao bado wana nia ya kurudisha utawala wa Man united wa kuchukua makombe na kusajili mastaa ambapo hivi sasa wanapambana kumuongezea mkataba kiungo Paul Pogba huku pia wakiangalia uwezekano wa kumsajili Eerlin Haaland anayechezea Borrusia Dortmund wakiamini staa huyo atavutika kucheza na Ronaldo timu moja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala