Connect with us

Makala

Nzengeli,Yao Kouasi Waachwa Dar

Wakati msafara wa klabu ya Yanga sc ukiondoka mapema asubuhi ya leo Januari 9 2024 kuelekea nchini Mauritania kwa ajili ya mchezo wa tano wa Klabu hiyo katika kundi A la michuano ya klabu bingwa barani Afrika imefahamika kuwa mastaa Maxi Nzengeli,Yao Kouasi Attouhoula na  Azizi Andambwile wameachwa jijini Dar es Salaam.

Mastaa hao wameachwa kutokana na kutokua fiti vya kutosha kushiriki katika mchezo huo wa kukata na shoka ambao klabu hiyo inatakiwa iondoke na alama ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kufuzu.

Meneja wa Idara ya habari ya klabu hiyo amesema kuwa wamewaacha wachezaji hao ili wapone kabisa majeraha hayo.

“Kutokana na ushauri ambao tumepatiwa na jopo letu la madaktari ni kuwa wachezaji wetu watatu Maxi Nzengeli, Kouassi Attohoula pamoja na Aziz Andambwile afya zao hazijaimarika”.Alisema Kamwe

“Wachezaji hao hawatokua katika mpango wa timu kuelekea kwenye mchezo wetu dhidi ya Al Hilal”.alimalizia kusema.

Yanga sc mpaka sasa ina alama nne za michuano ya klabu bingwa barani Afrika ikiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo wa Kundi A ambapo inapaswa kushinda michezo miwili ilyliyosalia ili kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala