Connect with us

Makala

Namungo Fc Yamvuta Mgunda

Klabu ya Namungo Fc imemuajiri kocha Juma Mgunda kuionoa klabu hiyo katika ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kuwa na mwenendo usioridhisha hali inayotishia nafasi ya klabu hiyo kubaki ligi kuu msimu ujao.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo inasema kuwa,Mgunda atachukua nafasi ya kuwa kocha mkuu sambamba na wasaidizi wake ambao ni Ngawina Ngawina,Shadrack Nsajingwa na Vladimir Niyonkuru.

Mgunda ambaye aliachana na Simba Queens wiki chache zilizopita anatarajiwa kuirudisha klabu hiyo kwenye nyakati za ushindi baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo mabaya msimu huu.

Mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini klabu hiyo ina alama sita pekee ikicheza michezo saba na inatarajiwa kukutana na Simba sc katika mchezo ujao wa ligi kuu ya Nbc siku ya Jumamosi Oktoba 25.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala