Klabu ya Simba iko katika hatua za mwisho kumsainisha mkataba mchezaji Kelvin Kapumbu (28) raia wa Zambia anayecheza klabu ya Zesco United sambamba na winga Joshua Mutale ambapo isajili huo unaosimamiwa na Crescentius Magori aliyekwenda nchini Zambia kuwanasa nyota hao.
Simba sc imeanza kufanya mabadiliko makubwa ya kiutawala ambayo sasa yanapelekea kufanya usajili wa maana kikosini humo huku Magori akipewa kazi kubwa ya kusimamia suala zima la usajili wa mastaa klabuni hapo.
Mutale ni winga mwenye miaka 22 akiichezea timu ya Power Dynamos ya nchini humo akitumika zaidi kama winga ama mshambuliaji wa kati namba mbili ambapo anasifika kwa kasi na kupiga mashuti imara anakuja Simba sc kuchukua nafasi ya Saido Ntibanzokiza ambaye klabu haijaonyesha nia ya kufanya mazungumzo ya mkataba mpya.
Pia usajili wa Kapumbu anayeichezea Zesco United ya nchini humo unakuja kuongeza machaguo zaidi eneo la kiungo cha chini huku pia ikitarajiwa kati ya Hamis Abdalah ama Sadio Kanoute mmoja anaweza kutemwa ili pia kutoa nafasi kwa sajili mpya za Kapumbu na Yusufu Kagoma ambao wote ni viungo wa ulinzi.
Magori anasifika kwa kupambana kupata mastaa wakubwa kuwaleta klabuni Simba Sc na ndie aliyeshiriki kwa kiasi kikubwa kuwasajili Meddie Kagere,Joash Onyango,Paschal Wawa na wakina John Bocco,Aishi Manula,Erasto Nyoni na Shomari Kapombe kutoka Azam Fc.