Connect with us

Makala

Djuma Shabani Anukia Coastal Union

Klabu ya Coastal Union yenye makazi yake jijini Tanga iko mbioni kukamilisha usajili wa beki wa zamani wa klabu ya AS Vita na Yanga Djuma Shaban kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa lengo la kuimarisha kikosi chake kuelekea kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Coastal imemsajili nyota huyo kama mchezaji huru baada ya kupita msimu mzima bila kuwa na timu ya kuitumikia Tangu aondoke Yanga sc ambapo taarifa zilisema angejiunga na Azam Fc huku akianza na mazoezi lakini kocha Yousouph Dabo alimkataa baada ya kutoona uhitaji wake kikosini humo.

Baada ya dili hilo kufeli Djuma aliondoka nchini na kurejea nyumbani kwao nchini Congo ambapo amekaa msimu mzima bila timu na hatimaye amerejea tena nchini kuja kukamilisha dili hilo.

Endapo staa huyo atafanya vizuri basi itakua rahisi zaidi kwake kurejea timu mkubwa za Simba sc,Yanga sc ama Azam Fc ambazo mara nyingi husajili wachezaji wanaoonekana kufanya vizuri katika timu ndogo kama ambavyo sasa makipa John Noble na Loy Matampi walivyo na soko kwa klabu kubwa ambazo zinapeleka ofa za kuwasajili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala