Connect with us

Soka

Mhilu sasa ni rasmi mali ya Simba SC

Baada ya purukushani na majibizano kati ya vilabu vya Simba SC na Kagera Sugar juu ya uhamisho wa mshambuliaji Yusuph Mhilu na kupelekea kukaribia kukwama,hatimaye amejiunga rasmi na wekundu wa Msimbazi.

Awali mchezaji huyo alitangazwa katika ukurasa rasmi wa Instagram wa Simba kabla ya Kagera Sugar kuja juu na kutishia kuishitaki klabu hiyo kutokana na kufanya hivyo kabla ya kufikia makubaliano ya bei ya mchezaji huo.

Lakini baada ya vikao vya muda mrefu hatimaye vilabu hivyo vimekubaliana ada ya Tsh milioni 40 hivyo Mhilu anaelekea kukipiga Msimbazi msimu ujao taarifa rasmi imetolewa na Kagera Sugar.

Usajili wa Mhilu huenda ukawa pigo kwa mshambuliaji wa Kibu Denis wa Mbeya City aliyekuwa akihusishwa kujiunga na mabingwa hao wa Tanzania Bara.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka