Connect with us

Soka

Manara akaribishwa na wazee Yanga

Msemaji mpya wa mabingwa wa kihistoria Tanzania Bara Haji Manara amekaribishwa rasmi makao makuu ya klabu hiyo Jangwani na wazee pamoja na viongozi mbalimbali timu hiyo katika tukio lilitokea hii leo.

Haji Manara baada ya kukaribishwa amesema kuwa ”ndugu zangu katika siku ngumu ni ambayo unapokewa na watu ambao unastahili kuwapokea,kwa mila na desturi zetu Afrika wazee wanapokewa na vijana,lakini kwa umaalumu mlionifanyia leo ni deni zito,sijawahi kupata mapokezi mazito kutoka kwa wazee wangu kama siku ya leo,deni hili pia ninalo kwa wanachama wote wa Yanga nchi nzima”.

Manara aliongeza ”nimerudi nyumbani sehemu ambayo imenikuza,mnafahamu wazazi wangu licha ya kucheza hapa lakini bado ni wanachama wa klabu hii na mimi kurudi hapa ni fahari kwamba narudi kufanya kazi katika klabu ambayo ilinilea na ndiyo klabu ya maisha yangu”.

Msemaji huyo pia aligusia malengo ya klabu hiyo kuwa ni kutwaa mataji kwenye mashindani ya ndani pamoja na kufika hatua ya makundi katika michuano ya klabu bingwa Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka