Connect with us

Soka

Liverpool,Madrid zashinda,PSG yavutwa shati UEFA

Michuano ya klabu bingwa Ulaya iliendelea tena usiku wa kuamkia leo ambapo Liverpool,Real Madrid na Man City ziliondoka na pointi tau muhimu katika michezo ya kwanza ya makundi.

Liverpool waliakuwa nyumbani iliwabidi kutoka nyuma na kupata ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya AC Milan,magoli ya Liverpool yalifungwa na Tomori aliyejifunga(dkk 9),Salah(dkk 49) na Henderson(dkk 69) hku yale ya AC Milan yakifunga na Rebic(dkk 42) na Diaz(dkk 44).

Real Madrid wakiwa ugenini Italia walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Inter Milan lililofungwa Rodrygo dakika ya 89,huku mabingwa wa EPL Manchester City wakiitandika RB Leipzig 6-3 katika mchezo uliojaa mvua ya magoli.

PSG licha ya kuwaanzisha mastaa wake Mbappe,Neymar na Messi kwa mara ya kwanza wameshindwa kupata ushidi baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Club Bruge ya Ubelgiji.

Matokeo mengine;

Atletico Madrid 0-0 FC Porto

Sporting 1-5 Ajax

Sheriff 2-0 Shakhtar Donetsk

Besiktas 1-2 Dortmund.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka