Connect with us

Soka

Liverpool,Arsenal zavuna pointi 3 EPL,City yang’ang’aniwa

Majogoo wa Anfield Liverpool imejikusanyia pointi tatu muhimu kwenye mechi yake ya tano ya ligi kuu soka nchini Uingereza baada ya kuichakaza Crystal Palace kwa mabao 3-0 katika dimba la Anfield.

Mabao ya Liverpool yaliwekwa kimianoi na Sadio Mane dakika ya 43 akimalizia mpira wa kichwa wa Salah uliomshinda mlinda mlango wa Palace Guaita,goli la pili lilifungwa na Mohamed Salah dakika ya 78 na goli la tatu lilifungwa na kiungo Naby Keita kwa shuti kali nje ya 18 ya box la Crystal Palace.

Liverpool wamepanda hadi nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi wakiwa na pointri 13 baada ya michezi mitano.

Washika bunduki wa London Arsenal nao wamepata ushindi wa pili mfululizo wa ligi hiyo baada ya kuifunga Burnley goli 1- katika dimba la Turf Moor na kufikisha alama sita katika mechi tano walizocheza.

Mabingwa wa ligi hiyo Manchester City wamelazimishwa suluhu na Southampton katika mchezo uliofanyoka katika dimba la Etihad,City hawakufanikiwa hata kupiga shuti moja lililolenga lango katika mchezo huo.Vijana hao wa Guardiola wana alama 10 katika michezo mitano.

Matokeo mengine kwa michezo ya leo;

Norwich city 1-3 Watford

Aston Villa 3-3 Everton

Wolvehampton 0-2 Brentford.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka