Connect with us

Soka

Liverpool waikazia FIFA kufungiwa wachezaji wake

Klabu ya Liverpool inaaminin kuwa sshirikisho la soka duniani FIFA hawana sababu ya msingi kuwafungia wachezaji wake kukosa michezo miwili mmoja wa EPL na mweingine wa klabu bingwa Ulaya.

Liverpool itawakosa wachezaji wake watatu mlinda mlango Alisson Becker,kiungo Fabinho na mshambuliaji Firmino baada ya kushindwa kuwaruhusu wachezaji hao kujiunga na timu yao ya taifa ya Brazil kwenye michezo ya kufuzu michuano ya kombe la dunia Qatar 2022.Liverpool na vilabu vingine vikubwa vya England vilifanya hivyo kutokana na vikwazo vya kusafiri baina ya mataifa hayo sababu ya UVIKO-19.

Siku ya Jumatano FIFA ilipokea maombi ya Brazil kuwazuia wachezaji wa EPL ambao hawakujiunga na timu ya taifa kutoshiriki michezo miwili ijayo na FIFA kukubali maombi hayo.

Liverpool wanaamini kutookana na hali ya UVIKO-19 duniani pamoja na sheria za karantini ingekua ngumu kwa wachezaji hao wakati wa kurejea England,hivyo wanaamini FIFA hawana sababu ya msingi wala haki ya kuwafungia wachezaji wake.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka