Connect with us

Soka

Kocha Singida Fg Ashikilia Hatma ya Banda

Kocha Mbrazil wa klabu ya Singida Fountain Gate Fc ameshikilia hatma ya usajili wa nyota wa zamani wa klabu ya Simba sc Peter Banda baada ya mabosi wa klabu hiyo kumuachia uamuzi wa mwisho kocha huyo ili kukamilisha dili hilo.

Nyota huyo raia wa Malawi ameshakubaliana kila kitu na mabosi wa klabu hiyo kuhusu kujiunga na klabu hiyo msimu huu wa dirisha dogo lakini uamuzi wa mwisho ameachiwa kocha Ricardo Ferreira kuamua kuwa asajiliwe ama lah kutokana na mipango yake.

“Mazungumzo ya awali yanaendelea vizuri lakini maamuzi ya mwisho yatabaki kwa benchi la ufundi kama litaridhia usajili wake ila kwetu viongozi hatuna wasiwasi na kiwango chake ila tunaheshimu watu kwa taaluma zao,” kimesema chanzo hicho.

Akizungumzia hilo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Singida, Olebile Sikwane amesema kwa sasa ni mapema sana kuzungumzia suala la usajili kwa sababu bado hawajakamilisha kwa asilimia zote, hivyo muda utakapofika kila kitu watakiweka wazi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka