Connect with us

Makala

Kocha Jkt Akabidhiwa Kilimanjaro Stars

Kocha wa timu ya Jkt Tanzania Ahmed Ally ameteuliwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania bara (Kilimanjaro Stars) ambayo imeingia kambini rasmi kujiandaa na michuano ya kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar kuanzia Januari 3 mwakani.

Tayari kocha huyo baada ya uteuzi ameshataja na kikosi cha mastaa takribani 29 watakaounda kikosi hicho.

Katika kikosi hicho hakuna staa wa Simba sc wala Yanga sc ambao wameachwa kutokana na timu hizo kuwa na michezo ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika kwa Yanga sc na michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika kwa Simba sc ambazo zote zitakua na michezo mwezi Januari.

Mastaa kutoka klabu za Azam Fc na Kagera sugar wametawala pamoja na wale wa kikosi cha Ngorongoro Heroes ambao wameitwa kwa ajili ya kupata uzoefu zaidi.

Mwaka huu timunza Taifa kutoka mataifa ya Zanzibar,Tanzania bara,Kenya,Uganda,Burundi na Burkina Faso zitashiriki michuano hiyo maalumu kuenzi siku ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Januari 12.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala