Connect with us

Soka

Kocha Hitimana asaini Simba SC

Aliyekua kocha wa Mtibwa Sugar Mrwanda Thiery Hitimana ametia saini katika klabu ya Simba kuwa kocha msaidizi wa mabingwa hao wa soka Tanzania Bara baada ya makocha wa timu hiyo kukosa sifa za kukaa benchi katika mechi za klabu bingwa Afrika.

Simba SC imeonekana ilijiandaa na kukabiliana na taarifa ya CAF katika orodha ya wakufunzi wasiokidhi vigezo ikiwepo kocha wake mkuu Didier Gomez kwa kumuajiri Hitimana.

Hitimana ana leseni ya CAF Diploma A inayotambulika na kuruhusiwa kukaa katika benchi la ufundi kwenye michuano iliyochini ya CAF na ameenda Simba kuhakikisha analiongoza benchi la Simba kipindi ambacho kocha mkuu Gomez akimalizia kozi yake ya UEFA Pro license itakayomruhusu kurudi tena na kuliongoza benchi hilo.

Mkufunzi huyo alikua ameshaanza kuifundisha Mtibwa Sugar katika maandalizi ya msimu mpya japo alikua bado hajasaini mkataba ambao alitarajiwa kuusaini pindi timu hiyo itaporejea makao yake makuu huko Manungu Morogoro,hivyo Simba wametumia nafasi hiyo kumsainisha haraka.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka