Connect with us

Soka

Kitambi Atua Geita Gold SC

Aliyekua kocha wa zamani wa klabu za Azam Fc na Namungo Fc Dennis Kitambi amejiunga na klabu ya Geita Gold Sc akichukua nafasi ya Hemed Morroco ambaye aliamua kujiuzuru kuifundisha timu hiyo yenye makazi yake mkoani Geita.

Kitambi alikua kocha wa Namungo Fc lakini alitimuliwa baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo mbaya ambapo sasa rasmi ametambulishwa kuwa kocha wa Geita Gold Fc.

Kitambi atakua na kazi kubwa ya kufanya kurejesha furaha kwa wakazi wa Geita baada ya timu hiyo kuwa na matokeo yasiyoridhisha katika ligi kuu nchini ambapo mpaka sasa ipo nafasi ya kumi ya msimamo ikiwa na alama 16 za ligi kuu.

Hata hivyo tayari kocha huyo ameanza na ushindi katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Singida Fountain Gate Fc baada ya kushinda 1-0 goli la Valentino Mashaka dakika ya 79 ya mchezo uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Nyankumbu mkoani Geita.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka