Connect with us

Soka

Lawi Afutiwa Kadi Nyekundu

Beki wa klabu ya Coastal Union Lameck Lawi amefutiwa kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya klabu ya Yanga sc baada ya kumvuta jezi kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Stephane Aziz Ki aliyekua akielekea kufunga.

Lawo alionyeskwa kadi hiyo dakika ya 70 ya mchezo huo ambao Yanga sc ilishinda 1-0 bao pekee likifungwa na Joseph Guede na kuihakikishia Yanga sc alama tatu za kufikisha alama 62 kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc.

Lawi amefutiwa kadi hiyo baada ya Kamati ya Uendeshaji wa Ligi kupokea taarifa za uchambuzi wa kitaalamu kutoka kwa wakufunzi wa waamuzi ambazo ziliainisha kuwa mchezaji huyo hakustahili kuonywa kwa kadi nyekundu badala yake alipaswa kuonywa kwa kadi ya njano kwani kulikuwa na mlinzi mwingine wa Coastal ambaye angeweza kufikia mpira.

Maamuzi hayo yamezingatia kanuni ya 12:8 ya Ligi Kuu kuhusu usimamizi wa Ligi kuu nchini huku Kanuni ya 42:1 (1, 1) ya Ligi Kuu kuhusu uthibiti wa waamuzi ikiwabana mwamuzi mkuu na msaidizi wake ambapo wamepewa onyo na kuwataka wawe makini wakiwa mchezoni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka