Connect with us

Soka

Kibu Asalimu Amri Simba Sc

Mshambuliaji Kibu Dennis amekubali yaishe baada ya kuamua kusalia klabuni Simba sc kwa miaka miwili zaidi ambapo siku chache zijazo atasaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kusalia klabuni hapo licha ya kuwa na ofa kutoka klabu zingine.

Kibu amekubaliana na ofa ya Simba sc ambapo atasaini mkataba huo wenye thamani ya shilingi milioni mia tatu ambazo zitalipwa kwa awamu huku akikubali kupokea mshahara wa milioni 12 kwa mwezi pamoja na bonansi mbalimbali kulingana na timu itakavyokua inapata ushindi.

Wawkilishi wa mchezaji huyo wamekubaliana na matakwa ya klabu ya Simba sc na kuachana na ofa ya milioni mia tano ya Ihefu na ile ya Yanga sc kwa maslahi mapana ya mchezaji ambapo Simba sc ana uhakika wa kucheza zaidi tofauti na kwingine ambao yatakua mazingira mageni kwake.

Yanga sc na Ihefu Fc pamoja na Azam Fc zilikua zinamuwania mchezaji huyo lakini zilimpa ofa na kumuacha achague mwenyewe kama atajiunga nazo ama lah ataamua kubaki Simba sc huku majaribio kadhaa ya mchezaji huyo kutaka timu hizo ziongeze dau yakigonga mwamba.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka