Connect with us

Soka

Kessy Atua Kmc

Beki Hassan Kessy amejiunga na klabu ya Kmc inayomilikiwa na Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumaliza mkataba na timu ya Mtibwa Sugar yenye maskani ya mjini Manungu mkoani Morogoro.

Beki huyo wa pembeni alijiunga na Mtibwa Sugar baada ya kuachana na klabu ya Nkana Red Devils ya nchini Zambia ambapo alichezwa kwa takribani msimu mmoja na kurejea nchini jana na sasa tayari amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Kmc huku akiwa tayari ameripoti kambini mkoani Morogoro kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu mpya.

Kessy ambaye ni mume halali wa mshambuliaji wa timu ya Taifa ya wanawake(Twiga stars) Asha Mwalala alijiunga,beki huyo amewahi kuichezea klabu ya Simba sc iliyomchukua kutoka Mtibwa Sugar kisha baadae akajiunga na Yanga sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka