Connect with us

Soka

Griezman Arejea Atletico Madrid

Mabingwa wa La Liga, Atletico Madrid wamefanikiwa kumsajili tena mshambuliaji, Antoine Griezmann kutoka Barcelona kwa mkopo Miaka miwili iliyopita mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alihama klabu hiyo baada ya Barca kulipa kifungu chake cha uhamisho wa pauni milioni 107.

Lakini wakati wa mchezaji huyo wa miaka 30 huko Nou Camp umekuwa wa kukatisha tamaa kwani alifunga mabao 35 katika michezo 102 na akashinda Ubingwa wa Copa del Rey pekee…. Amekuwa mchezaji wa 11 kuondoka Barcelona yenye shida ya kifedha msimu huu, pamoja na Lionel Messi aliyejiunga na Paris St-Germain.

Griezmann atakuwa mchezaji wa tatu kuuzwa siku ya mwisho ya uhamisho kutoka Barcelona. Mlinzi wa kulia Emerson Royal alijiunga na Tottenham kwa pauni milioni 25.8 na kiungo wa kati kijana Ilaix Moriba alihamia RB Leipzig kwa pauni milioni 13.7…Msimu uliopita Atletico ilimsajili mshambuliaji Luis Suarez kutoka Barcelona na aliisaidia timu ya Diego Simeone kushinda La Liga.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka