Shirikisho la mpira miguu duniani(FIFA) limetoa ruhusu ya wachezaji wa mataifa ya Amerika ya Kusini na Mexico waliokumbana na adhabu ya kufungiwa mechi mbili kutokana na vilabu vyao kutojiunga na timu zao za taifa kucheza michezo ya wikiendi hii pamoja na ile ya klabu bingwa Ulaya(UEFA).
Wachezaji wengi wa Kibrazil ndio walioathirika zaidi ya kadhia hiyo baada ya chama cha soka cha taifa hilo kupeleka maombi FIFA ya kuomba kufungiwa kwa wachezaji wake ambao hawakujiunga na timu ya taifa wakati wa michezo ya kufuzu kombe la dunia iliyofanyika hivi karibuni.
Lakini baada ya kikao kilichofanyika siku ya Ijumaa baina ya FIFA,FA ya England,vilabu na vyama vya soka vya Amerika ya Kusini na pamoja na nchi ya Mexico,FIFA imetoa uamuzi wa kuendelea kucheza kwa wachezaji wa mataifa hayo waliofungiwa kucheza michezo ya wikiendi hii baada ya Brazil na Chile kukubaliana kuyaondoa mashtaka yao FIFA.
Liverpool ndiyo ambayo ingeathirika zaidi kwa kukosa wachezaji wake watatu wa Kibrazil; Alison,Fabinho na Firmino hivyo ingekua pigo kubwa kwao.Wachezaji wengine walioruhusiwa kucheza ni Ederson na Gabriel Jesus(Man city & Brazil),Fred(Man Utd & Brazil),Raphina(Leeds Utd & Brazil),Almiron(Newcastle & Paraguay),Raul Jimenez(Wolves & Mexico) na Francisco Sierralta(Watford & Chile).